Yesu Ni Jina Nipendalo
Yesu ni jina nipendalo.
Napenda kulisikia;
Napenda kulitamka hilo,
Lililoniridhisha.
Chorus
Yesu, nakupenda,
Yesu, nakupenda;
Yesu, naktipenda,
Kwani ulinipenda.
Jina hilo huniambia,
Mwokozi alinipenda;
Damu yake ilimwagika,
Nipate kuokoka.
Lanionyesha sifa yake,
Iliyo katika Baba;
Njia ijapokuwa giza,
Yesu huniongoza.
Lanidhihirishia Yesu,
Aliyenihurumia;
Laondoa taabu yangu,
Niwe wake daima.
Home