Mle Kaburini

Mle kaburini, Yesu Mwokozi!
Alilazwa chini, Bwana wangu!

Bwana amefufuka,
Kifo kirneshindwa kabisa!
Gizani mie alitoka chini,
Sasa atawala huko mbinguni!
Yu hai! Yu hai!
Bwana Yesu yu hai!

Aungoja huo, Yesu Mwokozi!
Mchana ujao, Bwana wangu!

Walinda kaburi, Yesu Mwokozi!
Bure ni muhuri, Bwana wangu!

Kifo kimeshindwa, Yesu Mwokozi!
Pingu zimevunjwa, Bwana wangu'

Home