Rehema ya Baba Yetu
Rehema ya Baba yetu,
Yang'aza nchi yake;
Lakini ametuweka
Tuwe walinzi wake.
Chorus
Taa zenu na ziwake,
Nuru zenu tumeni;
Msafiri asizame,
Mwokoeni majini.
Giza ya dhambi twaona,
Mawimbi twasikia;
Wengine wanatafuta
Nuru za kutulia.
Taa zitengenezeni,
Mwokoeni msafiri;
Aangukaye majini,
Na asife gizani.
Home