Yesu Awakubali Wakosa
Yesu awakubali,
Wakosa, wahalifu,
Wambieni wa mbali
Habari ya wokovu.
Chorus
Tangazeni kwa bidli
"Akubali wakosa!"
Liwe neno dhahiri
"Akubali wakosa!"
Awakubali Bwana
Neno lake amini,
Watu kila aina,
Waje kwake tengoni.
Mimi ni safi moyo
Na mbele ya sheria,
Aliyesafi roho
Kwake ilitimia.
Akubali wakosa:
Nami anikubali:
Alivyonitakasa
Mbinguni niwasili.
Home