Nipe Pendo Sana
Nipe pendo sana,
Yesu Bwana,
Ndivyo niombavyo
Kwako sana;
Sikia Mwokozi
Ongeza mapenzi,
Nipe pendo sana Bwana.
Kwanza nilipenda
Ulimwengu;
Sasa nakupenda,
Bwana wangu;
Nakwomba Mwokozi,
Nijaze mapenzi,
Nipe pendo sana Bwana.
Na yaje mashaka
Na jeraha,
Yote ni baraka
Na furaha,
Nijuvye mapenzi
Zaidi, Mwokozi
Nipe pendo sana Bwana.
Utakapokufa
Moyo wangu,
Nami nikikwona,
Bwana wangu,
Kunikaribisha
Takupenda sana,
Takupenda sana Bwana.
Home