Nina Pumziko
Nina pumziko, maishani mwangu
Nafuraha tele ninayo,
Tangu niamue, kujisalimisha,
Kwa yesu yule wa ajabu
Ni wa maajabu, yehova yule mkuu
Hutukuzwa na malaika
Maselafi nao, wanamsujudu
Yesu yule wa maajabu
Msiwe na hofu, msiwe na shaka
Ninyi wana watakatifu
Maana tarubeta, itaitana
Ingieni rahani pangu
Upendo wangu, namutolea bwana
Ndiye chanzo cha imani yangu
Hunilisha vyema, malishoni bora
Kwa mito yenye maji hai
Sasa najitweka mikononi mwako
Ewe bwana uliyenifia,
Unipalilie na uniongoze, nifike uweponi mwako
Home