Uwe Huru Kutoka Dhambini

Uwe huru kutoka dhambini,
Uko uwezo wa ajabu;
Juu ya uovu uwe mshindi,
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Chorus
Uwezo wa ajabu ndimo
Damuni mwa Yesu,
Uwezo wa ajabu ndimo
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Uwe huru juu ya tamaa yako;
Uko uwezo wa ajabu;
Njoo, utakaswe katika mto,
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Uwe mwenye moyo safi mno,
Uko uwezo wa ajabu;
Alama itoke kwa uwezo,
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Ufanye kazi kwa Mfalme Yesu,
Uko uwezo wa ajabu;
Uishi dainia kumsifu,
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Home