Yesu Ataka Kianga

Yesu ataka kianga,
Kung'ara daima;
Kwa Yesu niwe kianga,
Po pote daima.

chorus
Kianga, kianga,
Kwa Yesu niwe kianga;
Kianga, kianga,
Niwe kianga kwake.

Niwe mpenzi wa Yesu,
Niwapende wote;
Kuwaonyesha wengine
Pendo siku zote.

Bwana Yesu, nimwulize
Anisaidie;
Moyo wangu utakaswe
Naye siku zote.

Niwe kianga kwa Yesu
Kuwa mwaminifu;
Nitumike naye Yesu,
Kisha nitamsifu.

Home