Jina Lake Yesu Tamu

Jina lake Yesu tamu.
Tukilisikia
Hutupoza, tena hamu
Hutuondolea. (X3)

Roho iliyoumia
Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia;
Raha, tukichoka. (X3)

Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata ungi,
Kwangu ni akiba. (X3)

Yesu, Mchunga, Rafiki,
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni. (X3)

Moyo wangu hauwezi
Kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana, zikubali. (X3)

Na utakaponiita,
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha
Kukusifu sana. (X3)

Home





Next song