Yesu kwa Imani
Yesu kwa imani,
Nakutumaini,
Peke yako;
Nisikie sasa,
Na kunitakasa,
Ni wako kabisa
Tangu leo.
Nipe nguvu pia
Za kusaidia
Moyo wangu;
Ulikufa Wewe
Wokovu nipewe
Nakupenda Wewe,
Bwana wangu.
Hapa nazunguka
Katika mashaka,
Na matata;
Palipo na giza
Utaniongoza
Hivi nitaweza
Kufuata.
Takuwa mzima
Nivushe salama
Mautini;
Sina hofu kamwe
Ukiwapo nami,
Nami nikwandame
Siku zote.
Home