Nina Raha kwa Mwamba Wa Imara
Nina raha kwa Mwamba wa imara,
Kwa teso langu naukimbilia;
Ni mwenye dhambi na niwe wako,
Mwamba wa Miaka, nafichwa kwako.
Chorus
Najificha, najificha,
Mwamba wa Miaka,
Nafichwa kwako.
Wakati wa amani ama huzuni,
Niliposhikwa na majaribuni,
Kwa shaka la maisha niende kwako,
Mwamba wa Miaka, nafichwa kwako.
Nilipolemewa katika vitani,
Nashika neema na tumaini;
Katika jaribu nasimama kwako,
Mwamba wa Miaka, naflchwa kwako.
Home