Peleka Jina La Yesu
Peleka jina la Yesu
Ko kote uendako;
Litafurahisha moyo,
Peleka uendako.
Chorus
Thamani, na tamu,
Ni jina lake Yesu;
Thamani, na tamu,
Ni jina lake Yesu.
Peleka jina Ia Yesu
Liwe silaha zako;
Utakapojaribiwa,
Lilia jina hilo.
Yesu, jina La thamani,
Limenifurahisha;
Nikiwasili mbinguni,
Atanikaribisha.
Kwa jina Ia Bwana Yesu,
Nimejiinamisha;
Ndiye Mfalme wa wafalme,
Katika ya maisha.
Home