Yesu, Msalaba Wangu

Yesu, msalaba wangu
Sasa nimejitweka,
Nikwandame Bwana wangu,
Wengine kuepuka.
Sina tamaa ya mali,
Mali ya ulimwengu;
Mimi ni tajiri kweli,
Ni mrithi wa Mungu.

Wajaponisumbua je,
Nitakukimbilia;
Mashaka yote na yaje,
Nitayavumilia.
Taabu hazinidhuru,
Nina mapenzi yako;
Na kwa haya nashukuru,
Napata yote kwako.

Moyo, pokea wokovu,
Kila siku wokoke;
Ushinde dhambi na hofu;
Subiri, utumike;
Roho yumo ndani yako,
Una pendo za Baba,
Mwokozi naye ni wako;
Mwenye hivyo, si haba.

Hima nawe, kaza mwendo:
Ujivike imani;
Hujafika mbingu bado.
Kwa Mungu tumaini:
Mwisho wa safari yako
Wasongea upesi;
Utakapofika huko,
Ni furaha halisi.

Home





Next song