Mpendao Bwana
Mpendao Bwana
Ije raha yenu!
Imbeni nyimbo za raha (2)
Wa ibada yenu. (2)
Chorus
Twenenda Zayuni,
Mji mzuri Zayuni;
Twenenda juu Zayuni,
Ni masikani ya Mungu.
Wasiimbe wao
Wasioamini,
Watoto wa Mungu ndio (2)
Waimbao chini. (2)
Twaona rohoni
Baraka za Mungu,
Tusijafika mbinguni
Kwenye utukufu. (2)
Tutakapomwona
Masumbuko basi,
Huwa maji ya uzima, (2)
Anasa halisi. (2)
Tupaze sauti,
Na yeshe machozi;
Twenenda kwa Imanweli (2)
Naye ni Mwokozi. (2)
Home