Namjia Yesu Nipumzike

Namjia Yesu nipumzike,
Kwa pumziko la wenye safi;
Nina kiu, nibarikiwe,
Nioshwe, nitakuwa safi.

Chorus
Yesu huokoa,
Damu yake yanitakasa,
Yesu huokoa,
Damu yake yanitakasa.

Dhambi zangu nazichukia,
Udhaifu wangu naona;
Natamani niokolewe,
Na damu yake nitakaswe.

Kwa Yesu namtolea yote,
Akiba na hazina zote;
Nahitaji baraka zake,
Nisafishwe damuni mwake.

Namtegemea Yesu pekee,
Naamini wokovu wake;
Damu yake imenitosha,
Sasa nimepata furaha.

Najawa na pendo la Mungu,
Na pendo Ia watakatifu;
Naimarishwa na uwezo,
Uwezo wa damu ya Kondoo

Home





Next song