Tazama Ishi Sasa

Ni ujumbe wa Bwana haleluya,
wa maisha ya daima,
Amenena mwenyewe haleluya,
utaishi ukitazama

Tazama, ishi sasa,
kumtazama Yesu,
Alinena mwenyewe, haleluya!
utaishi ukitazama

Uzima wa daima haleluya,
kwake Yesu utauona,
Ukimtazama tu haleluya,
wokovu u peke kwa Bwana

Ni ujumbe wa Bwana haleluya,
nawe shika rafiki yangu,
Ni habari ya raha haleluya,
mwenye kuinena ni Mungu.

Home





Next song