Ndiyo Damu ya Baraka

Ndiyo damu ya baraka
ituoshayo wakosa
Kwake Bwana twaokoka,
nasi twamsifu sasa;
Nimestahili hukumu,
siwezi kujitakasa
Nioshe katika damu,
takuwa safi kabisa

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu;
Takuwa safi kabisa.

Yesu alivikwa miiba,
na kuangikwa Mtini,
Na maumivu si haba
yaliyompata chini
Nataka kijito hicho
niende kuoga sasa
Ndicho kinitakasacho,
nami ni safi kabisa

Safi kabisa; safi kabisa!
Ndicho kinitakasacho,
Nami ni safi kabisa.

Baba, kweli nimekosa,
moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi ni nyingi kabisa,
nipate wapi wokovu?
Yesu kijitoni pako naja
naamini sasa
Nioshe kwa damu yako,
takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe kwa damu yako,
Takuwa safi kabisa.

Home





Next song