Ati Twonane Mtoni?
Ati twonane mtoni?
Maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.
chorus
Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika mtoni
Penye kiti cha Mungu.
Tukitembea mtoni
Na Yesu Mchunga wetu;
Daima tu ibadani
Usoni pake kwetu.
Tukisafiri mtoni
Tutue ulemeao
Wema wa Mungu yakini:
Una taji na vao!
Home
Next song