Jina La Yesu, Salamu!
Jina Ia Yesu, salamu!
Lisujudieni,
Ninyi mbinguni, hukumu
Na enzi mpeni.
Enzi na apewe kwenu,
Watetea dini
Mkuzeni Bwana wenu
Na enzi mpeni.
Enyi mbegu ya rehema
Nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi mpeni.
Wenye dhambi kumbukeni
Ya Msalabani
Kwa furaha msifuni
Na enzi mpeni.
Kila mtu duniani
Msujudieni,
Kote-kote msifuni
Na enzi mpeni.
Sisi na wao pamoja
Tu mumo sifani
Milele sifa ni moja,
Ni "Enzi mpeni."
Home