Katika Yesu Sina Shaka

Katika Yesu sina shaka,
Yeye amenitosha;
Pendo lake lanipendeza,
Kwake nina ushirika.

chorus
Katika Yesu sina shaka,
Amenilinda po pote;
Kwangu Neno lake limetimizwa,
Kwake sina shaka lo lote.

Katika Yesu sina shaka,
Ingawa nina haja;
Hunifariji na upendo,
Ajua kufurahisha.

Katika Yesu sina shaka,
Na ameniridhisha;
Yeye tayari kuniponya,
Kwake nimefadhilika.

Home





Next song