Ni Siku Kuu
Ni siku kuu siku ile
Ya kumkiri Mwokozi!
Moyo urnejaa tele,
Kunyamaza hauwezi.
Chorus
Siku kuu! siku kuu!
Ya kwoshwa dhambi zangu kuu
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Siku kuu, siku kuu!
Ya kwoshwa dhambi zangu
Tumekwisha kupatana
Mimi wake, Yeye wangu,
Na sasa nitamwandama,
Nikiri neno la Mungu.
Moyo tulia kwa Bwana,
Kiini cha raha yako.
Huna njia mbili tena:
Yesu ndiye njia yako.
Nadhiri yangu ya mbele
Nitaiweka daima,
Hata ije siku ile
Ya kwonana kwa salama.
Home