Rafiki Wa Yesu Ndimi
Rafiki wa Yesu ndimi,
Niliye dhaifu;
Ninaye Rafiki mwema,
Aliyekomboa.
Yesu Mshirika,
Rafiki yangu;
Ushirika mtakatifu,
Ndiye Rafiki yangu.
Urafiki wa daima,
Usiopunguka;
Yesu anipa amani,
Yu Mwenye hakika.
Aniongoza gizani,
Aijua njia;
Anilinda maishani,
Aliyenifia.
Nikishikwa na ugonjwa.
Ataniinua;
Kifo nikikaribia
Ataniongoza.
Yesu ni Rafiki Mwema,
Humu duniani;
Yeye atanichukua
Mpaka mbinguni.
Home