Nichungue Mungu

Nichungue, Mungu unijue,
Unijaribu niangalie;
Zitambue dhambi zangu zote,
Unitakase na uniweke.

Nakusifu, urnenisafisha,
Neno lako litimike sasa;
Unijaze na moto wa mbingu,
Unipe matumaini yangu.

Unitwae, kweli niwe wako,
Unijaze na upendo wako;
Uondoe kiburi na choyo,
Bwana, nakujitolea moyo.

Mungu Roho, una ufufuo,
Kwangu ianzishe kazi yako;
Haja zote zitapatanika,
Bwana, naomba kwako baraka

Home