Waimba Sikizeni
Waimba, sikizeni,
Malaika mbinguni;
Wimbo wa tamu sana
Wa pendo zake Bwana:
"Duniani salama,
Kwa wakosa rehema. '
Sisi sote na twimbe
Nao wale wajumbe;
Waimba, sikizeni,
Malaika mbinguni.
Ndiye Bwana wa mbingu,
Tangu milele Mungu,
Amezaliwa mwili,
Mwana wa mwanamwali;
Ametoka enzini
Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie,
Iii tusipotee,
Waimba, sikizeni,
Malaika mbinguni.
Seyidi wa amani
Arnetoka mbinguni,
Jua la haki, ndiye
Atumulikiaye;
Amejivua enzi,
Alivyo na mapenzi,
Ataka kutuponya,
Kutuzalisha upya,
Waimba, sikizeni,
Malaika mbinguni.
Njoo upesi, Bwana,
Twakutamani sana;
Kaa nasi, Mwokozi,
Vita hatuviwezi;
Vunja kichwa cha nyoka,
Sura zako andika,
Tufanane na Wewe,
Kwetu sifa upewe,
Waimba, sikizeni,
Malaika mbinguni.
Home