Niwonapo Mti Bora
Niwonapo Mti bora
Kristo aliponifia
Kwangu pato ni hasara,
Kiburi nakichukia.
Na nisijivune, Bwana,
Ila kwa mauti yako;
Upuzi sitaki tena,
Zi chini ya damu yako.
Tangu kichwa hata nyayo
Zamwagwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo,
Pendo zako zimetimu.
Vitu vyote vya dunia
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zaniwia
Nafsi, mali, na maisha.
Home