Mungu Aliahidi
Mungu aliahidi,
Na kwa fadhili yake;
Tutapata pumziko,
Katika mkono wake.
chorus
Tukiona mashaka mengi,
"Tulia", amri yake,
Roho yangu ina amani,
Katika mkono wake.
Ijapo hufahamu,
Na usifadhaike;
Hutasumbuka tena,
Katika mkono wake.
Na ukishughulika,
Kwa mambo siku zote;
Roho itapumzika,
Katika mkono wake.
Furaha ya ajabu,
Tena amani yake;
Zimewekwa tayari
Katika mkono wake.
Home