Mungu Mtukufu Aliye Bwana
Mungu Mtukufu aliye Bwana,
Akamtoa Yesu Mpendwa Mwana;
Akawa dhabihu kwa dhambi zote,
Kufungua njia kwa watu wote.
Chorus
Msifuni, msifuni,
Nchi imsikie;
Msifuni, msifuni,
Bwana mshangilie:
Njoni kwake Baba
Kwa Yesu Mwana,
Mpeni heshima
Aliye Bwana.
Ukombozi wetu, tendo Ia Mungu,
Ni ukamilifu kwa kila mtu;
Mwenye ukosefu akimwamini,
Atasamehewa na Yesu, kweli.
Ametufundisha mambo ya mbingu,
Tukafurahishwa na Mwana Mungu;
Ametuinua tukae naye,
Atatuongoza hata milele.
Home