Upendo Wa Yesu Ni Wa Ajabu

Upendo wa Yesu ni wa ajabu,
Alitoka mbinguni;
Akashuka kuonja umaskini,
Akateswa hapo msalabani.

chorus
Upendo, nilioupewa,
Neema, isiyopunguka;
Upendo, Upendo,
Nitautangaza upendo.

Si kwa haki yangu niliyotenda.
Bali kwa pendo lake;
Sistahili neema wala pendo
Yesu hunipa wokovu wake.

Yesu atanilinda safarini,
Kwa maishani mote;
Sitaona shaka wala hasara,
Anatimiza ahadi zote.

Home