Mungu Baba Yangu, U Mwaminifu,
Mungu Baba yangu, U Mwaminifu,
Hakuna geuzo ndani yako;
Hubadiliki, wewe ndiwe sawa,
Jana, leo na siku zijazo.
chorus
Wewe Mwaminifu,
Wewe Mwaminifu,
Kila siku fadhili napewa;
Vitu vyote ninavyo umenipa,
Wewe Mwaminifu kwangu Bwana.
Na viumbe vyote hulingamana,
Kuonyesha utukufu wako;
Jua, na mvua, mwezi tena nyota
Hulishuhudia pendo lako.
Samaha la dhambi, tena amani,
Hivi vyote ni baraka zako;
Nguvu zako zitadumu milele,
Nimebarikiwa sasa kwako.
Home